Header Ads

Header ADS

Kufuatia ajali ya Lori la Mafuta Msemaji wa Serikali atoa Neno

Dkt.Hassan Abbas ambaye ni msemaji Mku katika Serikali amesemaq kuhusu ajali ya Lori la Mafuta iliyotokea Morogoro na kusababisha vifo zaidi ya Watanzania 57 pamoja na wengine zaidi ya 70 kujehuriwa vibaya.Amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa kuhusu ajali hiyo.











Pia,Dkt Abbas amesema kuwa timu ya uokoaji na Mkuu wa Mkoa wanaendelea kukabilia na hali katika eneo la tukio
''Tumepokea kwa masikitiko  taarifa kuhusu ajali ya Lori la mafuta,Morogoro,iliyosababisha moto na kuunguza baadhi ya watu kadhaa.Mkuu wa Mkoa na timu ya uokoaji wanaendelea kukabiliana na hali katika eneo la tukio.Taarifa kamili kuhusu idadi ya vifo na majeruhi itatolewa badae''.Ameandika Dkt Abbas kwenye ukurasa wa Twitter.
  Hata hivyo,ameendelea kusema kuwa''Tunaendelea kutoa wito kwa Wananchi kukaa mbali na eneo la ajali hasa yanapohusika magari na vyombo vingine vya usafiri vilivyobeba vitu vinavyoweza kuripuka kama mafuta''.
  Aidha,Lori  hilo likiwa linatokea Dar es salaam limebeba mafuta na lilipofika Itigi,Morogoro likiwa katika hali ya kumkwepa Bodaboda aliyekatiza mbeleyake ndipo Lori hilo likaanguka.
 Mara baada ya Lori hilo kuanguka watu mbalimbali wakiwemo Bodaboda waliwasili katika eneo la ajali kwa kudhumuni la kuiba mafuta yaliyokuwa yakimwagika,moto ulilipuka na zaidi ya watu 57 kuaga dunia na wengine kujeruhiwa vibaya kutokana na mlipuko huo.
   Kwa mujibu wa Kamanda wa Polis Mkoani Morogoro,ameeleza kuwa ajali hiyoimetokea mita 200 kutoka kituo kikuu cha Mabasi cha Msamvu ukitokea Dar es salaam.

No comments

Powered by Blogger.