Header Ads

Header ADS

Kuhusiana na kesi ya Lisu kaka yake afunguka kuwa,'Hii kesi sio ya ovyo'

  Alute Mughwai kaka yake aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo[CHADEMA] Tundu Lissu ameeleza kuwa Kesi ya maombi iliyofunguliwa na lissu sio ya hovyo kama inavozungumziwa na upande wa Serikali.
   Baada ya majibizano makali ya kisheria kutokea mahakamani,Mughwai amesema hayo jijini Dar es salaam ambapo Upande wa Serikali ulipeleka Mawakili 15 kwaajili ya kuweka pingamizi dhidi ya kesi hiyo.












  Aidha kwa mujibu wa Mughwai ameeleza kwamba kesi hiyo ina umuhimu mkubwa pia ya kipekee kulingana na Mustakabali wa Nchi ndiyo maana upande wa Serikali imepeleka Mawakili 15 ikiwa ni pamoja na Mwanasheria Mkuu.
  ''Tunataka mahakama itueleze kama ni sahihi kwa Mbunge wa Bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushambuliwa mchana kweupe,halafu hapewi huduma ya matibabu,baada ya hapo anaondolewa Ubunge,kwa hoja ya kwamba hayupo Bungeni na hawajui alipo''.Mughwai amesema.
     Hivyo basi,kutokana na upande wa Serikali kuwasilisha pingamizi la awali lenye hoja 9 kutaka shtaka hilo lifutiwe mbali,maombi hayo ya Lissu ambayo yalitakiwa kusikilizwa hapo jana mbele ya Jaji Sirilius Matupa hayakusikilizwa.

No comments

Powered by Blogger.