Majaliwa aeleza namna maonesho ya wiki ya viwanda SADC yatakavo fungua milango mingi ya masoko
Waziri Mkuu Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania,Kassim Majaliwa amewaeleza Watanzania kuchangamkia fursa zipatikanazo kupitia maonesho ya Viwanda ya Nchi Wanachama Wa Jumuiya Ya Maendeleo Ya Nchi za Kusini Mwa Afrika[SADC] ili kusaidia ukuaji wa Uchumi wa Viwanda unaojengwa na Serikali.
Hayo amesema mara baada ya kufanya Ziara yake ya kutembelea maonesho hayo yanayofanyika katika kituo cha Mikutano Cha Kimataifa cha Julius Nyerere,Viwanja vya Karimjee na Gymkana ambapo amesema maandalizi ya Mkutano Mkuu 39 wa Wakuu Wa Nchi za SADC yamekamilika yakihusisha kuwepo kwa maonesho ambayo Nchi Wanachama Wataonyesha Teknolojia,Ubunifu na bidhaa zao kutoka katika Viwanda vya Nchi za SADC.
Majaliwa ameeleza kuwa Serikali imewapa fursa Wafanyabiashara wakubwa,wa kati pamoja na wadogowadogo pia wanaozalisha bidhaa kwa mikono kuja kuonyesha ili kuweza kupata Teknolojia kutoka kwa wageni ambao wapo Nchini.
''Sisi kama Serikali tumetoa fursa kwa wale ambao wanafanya kazi na kuzalisha bidhaa zao kwa kutumia mikono kuja kuonyesha bidhaa zao ili ziweze kupata masoko kwa Nchi Wanachama wa SADC kwani Nchi zote zinakuja hapa kuleta bidhaa mbalimbali kwahiyo Watanzania wanatakiwa kutumia fursa hii ili kuwauzia wageni bidhaa zetu''.Amesema Majaliwa.
Pia,Majaliwa amesema maonesho haya ni muhimu na lengo kubwa la kuzikutanisha Nchi za SADC kuja Tanzania ni kuonyesha bidhaa,Teknolojia za uzalishaji viwandani pamoja na ubunifu wa uzalishaji bidhaa hizo kwa Watanzania ambao hawaja wahi kufika Namibia,Msumbiji,Malawi pamoja na Nchi zingine za kusini Mwa Afrika ni fursa kubwa kuleta bidhaa zao ili kupata soko la SADC.
''Maonyesho haya ya wiki ya viwanda kutoka Nchi wanachama wa SADC yanafursa nyingi kwa Watanzania kwani yatafungua milango mingi ya masoko kwa bidhaa zinazozalishwa Nchini pia yatakuwa kwa wazi kwahiyo Watanzania wanatakiwa kutumia fursa hii kubwa kuona bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa Nchini na Nchi wanachama kutoka jumuiya hii''Majaliwa amesisitiza.
Vilevile Majaliwa ameendelea kusema kuwa mkutano huu ni fursa kwa Watanzania kutangaza vivutio vya Watalii vilivyopo Nchini ili kuweza kuboresha Sekta hiyo na kuwezesha wageni kutoka Nchi Wanachama wa SADC kuja kwa wingi kuwekeza Nchini.

No comments
Post a Comment