Header Ads

Header ADS

Watu 95,wajeruhiwa kutokana na shambulizi la kundi la Taliban huko Nchini Afghanistan katika mji wa Kabul.

Serikali Nchini Afghanistan imesema mlipuaji wa kujitoa mhanga amelipua bomu ndani ya gari leo na kujeruhi watu 95.
      Maafisa wakuu wa Serikali Nchini Afghanistan wamesema kuwa mlipuaji wa kujitoa mhanga amelipua bomu lililokuwa limetegwa ndani ya kituo kimoja cha polisi katika mji mkuu wa Nchi hiyo Kabul siku ya jumatano na kujeruhi watu 95.
      Mlipuko mkubwa uliosababishwa na shambulizi hilo umepelekea mamia ya watu kujeruhiwa.Kundi la Taliban limekubali kuhusika katika shambulizi hilo.Hakukuwa na uthibitisho wa mara moja kuhusu vifo vyovyote katika shambulizi hilo la pili katika Mji mkuu wa Afghanistan katika muda wa siku chache zilizopita.











Firdaus Faramarz ambaye ni msemaji wa polisi ameliambia Shirika la habari Associated Press kuwa mlipuaji huyo,alilipua bomu nje na makao makuu ya polisi.Kundi la Taliban limesema kuwa dhumuni kubwa lilikuwa ni kilipua kituo cha kuwasajili maafisa wa vikosi vya usalama kilichopo katika eneo hilo.Katika eneo la Kabul Vyombo vya habari Nchini humo vilionyesha moshi mkubwa ulionea katika makazi ya jamii ya walio wachache ya Hazara.
    Mwaka 2017 Kundi hilo lilifanya shambulizi katika makuu hayo makuu ya polisi ambapo lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 20.Afisa Mtendaji mkuu wa Serikali Abdullah Abdullah katika ujumbe kupitia mtandao wa Twiter amelaani shambulizi hilo na kudai kuwa dhumuni la magaidi hao ni kukatiza kampeni za uchaguzi wa Rais.
     Kutokana na sababu za usalama Nchini Afghanistan imepelekea kuchelewa kwa uchaguzi wa urais ambao unatarajia kufanyika Septemba 28.
      Kundi hilo la Taliban lilitoa onyo siku ya jumanne katika ushiriki wa uchaguzi kwa raia wa Afghanistan na kijiepusha katika mikutano ya kampeni za uchaguzi ambayo wenda italengwa.
       Nchini Afghanistan ambapo kundi hilo limekua likifanya mashambulizi ya karibu kila siku kwa lengo la kushambulia vikosi vya kijeshi vya serikali na maafisa wa serikali ama wale wanaoonekana kuegemea upande wa serikali.
       Baada ya utengano Nchini Afghanistan hata baada ya kundi la Taliban na Marekani kuonekana kuwa karibu kufikia mkataba wa kihistoria na Marekani kuondoa vikosi vya kijeshi ili kundi hilo liweze kuweka ahadi kuwa nchi hiyo haitatumiwa kama ngome ya kupanga mashambulizi ya wanamgambo.

No comments

Powered by Blogger.