Waziri Wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais Muungano na Mazingira Simbachawene apongeza Mradi wa upandaji mikoko Zanzibar
Waziri wa nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira George Simbachawene ameupongeza mradi wa utunzaji mazingira kupitia upandaji wa miti ya mikoko visiwani Zanzibar
Simbachawene ameupongeza mradi huo Agost 5,2019 akiwa kwenye siku ya kwanza ya ziara yake ya kujitambulisha na kufanya ukaguzi wa miradi ya muungano na mazingira visiwani humo.
Waziri huyo amesema kwamba amefurahishwa na utendaji wa kazi wa Ofisi ya makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar katika utekelezaji wa mradi huo pamoja na ufadhili kutoka Shirika la Mazingira la Umoja Wa Mataifa [UNEP].
''Niwapongeze sana kwa mradi huu mzuri na tunaona matokeo yake umesaidia mawimbi yasije kwa kasi katika eneo hili na kusababisha mmomonyoko na tukiamua kufanya kazi kwa pamoja na jamii tunaweza kufanya vizuri''.Hayo yamesemwa na Simbachawene.
Pia,Simbachawene ametoa fursa kwa wataalam kuangalia njia nyingine za kuweza kugundua miradi mingine katika mikoa yenye fukwe kama vile Dar es salaam,Tanga,Lindi na Mtwara ili kusaidia katika utunzaji wa mazingira.
Kwa upande mwingine amekagua Ujenzi wa kituo cha afya Kianga kilichopo Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi na kutoa pongezi kwa Wananchi katika kusimamia Mradi huo.
''Nawapongeza sana Wananchi hasa kwa kamati hii mmefanya vizuri kusimamia Mradi huu wa Ujenzi wa kituo cha Afya tunaamini udokozi haukuwepo kazi imefanyika fenicha [samani] zipo,vifaa tiba na utendaji kazi mzuri unaoendelea kufanyika''Ameongeza Simbachawene

No comments
Post a Comment