Header Ads

Header ADS

Kaimu Kocha mkuu wa Taifa Stars Ndayiragije aweka wazi kikosi cha wachezaji 25,

       Ettiene Ndayiragije ambaye ni kaimu kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars ameweka baina kikosi cha wachezaji 25,kitakachowasili leo jumatatu kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi dhidi ya Sudan ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa kupambania kufuzu fainali ya Mataifa bingwa Afrika[CHAN].
    Ni mchezo ambao Stars itakuwa katika uwanja wa nyumbani jijini Dar es salaam ifikapo wiki hii mwishoni,lakini pia katika mchezo wa mkondo wa pili utakwenda kumalizika mwezi ujao mjini Khartoum ambapo kama itaibuka na ushindi itajikatia tiketi ya kwenda kushiriki fainali za CHAN zitakazochezwa Nchini Cameroon hapo mwakani.


No comments

Powered by Blogger.