Header Ads

Header ADS

Tanzania yapewa ujumbe kutoka umoja wa Mataifa

Dkt.Amina Mohamed ambaye ni Naibu Katibu wa Umoja wa Mataifa(AU) ametoa ushauri kwa nchi ya Tanzania kuendelea kuimarisha amani katika ukanda wa Maziwa makuu pamoja na kuendelea kutoka askari wake ili kuungana na vikosi vya ulinzi na amani duniani.
  Aidha Dkt.Mohamed  ametoa wito huo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa  Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Palamagamba kabudi New york Marekani.











Pia,ameongeza kuwa AU inatambua mchango wa Tanzania katika ulinzi wa amani duniani na kwamba upo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza jitihada hizo ili dunia kuzidi kuwa sehemu salama ya makazi na maisha ya viumbe.
  “Tanzania imekuwa muhimili muhimu katika kuhimiza amani katika ukanda wa maziwa makuu ikiwa ni pamoja na kuhifadhi wakimbizi kutoka ukanda huo kwa miaka mingi bila kuchoka,” alisema Dkt. Mohammed.
  Kabudi amesema kuwa Tanzania inatambua nafasi ya umoja wa mataifa na kwamba itaendelea itasalia kuwa mwanachama katika umoja huo.
Napenda kukuhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kutoa askari wake katika vikosi vya ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani,” alisema Prof. Kabudi.
  Aidha kabudi ameeleza hatua mbalimbali ambazo Tanzania imepiga katika masuala ya maendeleo endelevu(SDGs) ikiwa ni pamoja na afya,maji,ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi pamoja na masuala ya kuimarika kwa demokrasia nchini.
  Prof. Kabudi amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Marekani alipokuwa akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
   NA MWANDISHI WETU,FATMA MAULID
    
   

No comments

Powered by Blogger.