Header Ads

Header ADS

Waziri ashauri Wananchi kupunguza Matumizi mabaya ya Pombe

Ikiwa leo ni Oktoba 03,2019 Siku ya kuadhimisha upingaji wa unywaji pombe duniani wananchi wameshauriwa kupunguza matumizi mabaya ya pombe ili kuepuka ajali mbalimbali kama ajali,magonjwa na ukatili wa kijinsia.
   Hayo yamezungumzwa leo na Naibu Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto ndugu Dkt Faustine Ndugulile wakati alipohudhuria maadhimisho hayo ambalo limeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali linalopinga matumizi ya pombe TAAnet ambapo amewashauri watu kupunguza matumizi ya pombe kwani yana madhara mengi.













Pia amezitaka mamlaka husika kuchkua sheria kali kwa wale wote wanaouza pombe kiholela na kwa wale wate wanaouza pombe bila leseni kusakwa na kukamatwa.
   Anna Baraka ambaye ni Afisa Maendeleo ya jamii Kata  Kising’a Mkoa wa Iringa amesema kuwa katika kata yake watu wengi walikuwa wanatumia muda mwingi kunywa pombe bila kufanya kazi za maendeleo huku akisema baada ya kupata elimu kwa sasa wamepunguza unywaji wa pombe.
  Hata hivyo shirika hilo linalopinga matumizi ya pombe TAAnet  lina dhumuni  ya kutetea kushawishi na kutekeleza sera madhubuti ya serikali ya kupinga matumizi mabaya ya pombe.
 NA MWANDISHI WETU,DIANA MALEKELA.

No comments

Powered by Blogger.