Header Ads

Header ADS

Wanafunzi 14 wapigwa viboko na Mkuu wa Mkoa.

     Albert Chalamila ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya achukua hatua ya kuwacharaza viboko wanafunzi wa mara baada ya kubaini kuwa wanafunzi hao wanamiliki simu kinyume na sheria za shule katika shule ya Secondari Kiwanja iliyopo Mkoani Mbeya katika wilaya ya Chunya.
  Ambapo wanafunzi hao mnamo Octoba mosi 2019 walijihusisha  na uchomaji moto mabweni mawili katika shule hiyo wakiwa na lengo la kulipiza kisasa mara baada ya kunyang'anywa simu huku kuhusu tukio hilo wanafunzi wa tano wakishikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya maojiano.











Elly Mnyarape ambaye ni mkuu wa shule hiyo ameeleza mnamo Septemba 30 majira ya mchana simu 26 zilikamatwa shuleni hapo mara baada ya kufanyika kwa msako na kufuatia kuteketezwa kwa mabweni siku ile ile majira ya usiku.
    Chalamila alichukua uamuzi huo mara baada ya kutembelea shule hiyo na kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa shule kuwa baadhi ya wanafunzi wanamiliki simu kinyume na sheria.
    Hata hivyo,chalamila baada ya kuwaadhibu wanafunzi hao amemueleza mkuu wa shule hiyo kuwa ili wanafunzi wengine wapate fundisho anapaswa kuchukua hatua za kinidhamu kwa wanafunzi hayo.
     Aidha,Chalamila ameagiza jeshi la polisi kuhakikisha wazazi wa watoto hao waliokutwa na simu kila mmoja analipa shilingi milioni moja zitakazotumika kukarabati mabweni hayo yaliyoteketezwa.
   Lakini pia,katika mitandao ya kijamii imesambaa video ikionyesha tukio nzima la Chalamila pindi akiwa anawaadhibu wanafunzi hao kwa kosa la utovu wa nidhamu katika shule hiyo.
        Imetolewa na mwandishi wako; Adolf Mwingira

No comments

Powered by Blogger.