Header Ads

Header ADS

Tundu lissu asaini mkataba maalumu na kampuni maalumu ya kisheria

Tundu lissu ambaye ni Mbunge wa zamani wa Singida Mashariki amesaini mkataba maalumu na kampuni ya kamataifa ya kisheria Ya Amsterdam and Partiners LPP akiwapa jukumu la kusimamia haki zote za kikatiba na za kimataifa.
     Kampuni hiyo imeeleza kuwa imefurahi kufanya kazi na Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha  Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).











“Tunajivunia kufanya kazi na Tundu Lissu katika kuongeza uelewa kwenye hali yake na kampeni dhidi ya uvunjifu wa sheria na haki za kisiasa,” imeeleza kampuni hiyo.Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji tangu Januari 6, 2018 alipoenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na kujeruhiwa kwa risasi, alitangaza kuahirisha kurejea nchini Septemba 7 mwaka huu kama alivyoahidi ili akutane kwa mara nyingine na madaktari wake.
   Mwanasiasa huyo alisambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 07,2017 akiwa maeneo ya nyumbani kwake Area d Dodoma.
     Aidha Alipatiwa matibabu ya awali katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kisha akapelekwa jijini Nairobi kwa matibabu zaidi, kabla ya kuhamishiwa nchini Ubelgiji alikoendelea kupatiwa matibabu hadi leo.odoma.
Pia Kampuni ya Amsterdam and Partners LLP yenye makazi yake jijini London nchini Uingereza, kazi yake kubwa ni kuwashauri wateja hususan kwenye changamoto kubwa za kisheria zinazojitokeza.

   

   

No comments

Powered by Blogger.