Header Ads

Header ADS

Viongozi wa CCM wakutana na TGNP Mtandao kwa lengo la kujadili ushirika wa wanawake katika uongozi Wilayani Kishapu.

    wajumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeendesha mkutano na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao) kujadili ushiriki wa wanawake katika kuwa nia nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wilayani Kishapu.
    Mkutano huo umefanyika leo Oktoba 27, 2019 kwenye Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Maganzo wilayani Kishapu, ambao ulihudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya siasa ya CCM wilayani humo, ambayo inaongozwa na Mwenyekiti Shija Ntelezu.
    Ambapo Mwenyekiti wa  CCM wilayani Kishapu Shija Ntelezu,akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo ameupongeza mtandao huo wa jinsia Tanzania (TGNP Mtandao), kwa kutoa elimu za kuhamasisha wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi ili kuleta usawa wa kijinsia kwenye nafasi za uongozi.

    














                                                                                Amesema kipindi cha nyuma wanawake walikuwa hawajitokezi kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi, lakini sasa hivi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi, na kubainisha chama hicho wilayani humo kimejiwekea mikakati ya kuwapatia kipaumbele wanawake ambao watakuwa wakitia nia ya kutaka uongozi.
    “Nalipongeza sana Shirika hili la TGNP Mtandao kwa kutoa elimu kwa wanawake kujitokeza kushiriki kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi, ili kufikia 50 kwa 50 kwenye nafasi za uongozi, ambapo na sisi kama CCM tumekuwa tukiliunga mkono, na ndio maana mwanamke akayetia nia tunampa kipaumbele,”amesema Ntelezu.
       Naye mjumbe wa kamati ya siasa CCM wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo , amesema chama chao kinathamini sana usawa wa kijinsia, na kutolea mfano katika vijiji 117 wilayani humo ambapo kati ya vijiji 25 ambavyo walijitokeza wanawake kuchukua fomu za kuwania nafasi za uenyekiti wa kijiji, kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 24,2019 wamewapitisha wote kugombea nafasi hizo.

Amesema hata katika nafasi za kuwania ujumbe, kama kuna watu nane wanataka nafasi hiyo wakiwemo na wanawake wawili, lazima wapitishwe wanawake hao, na baada ya hapo ndipo wanaanza kuchagua wanaume ili kujazia nafasi.

Aidha mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) CCM wilayani Kishapu Rahel Madundo, amewapongeza wanawake ambao wamejitokeza kuwa nia nafasi za uongozi kweye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu, na kutoa wito pia wajitokeza kuwania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu mwakani.

Kwa upande wake Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao EvaHawa Juma, amesema wameendesha mkutano huo na wajumbe wa kamati hiyo ya Siasa ya Chama Cha mapinduzi CCM wilayani Kishapu, ambapo jana wamefanya na vyama vingine vya siasa, na kubainisha lengo lake kubwa ni kutoa nafasi kwa wanawake kushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi.

Amesema wanawake wamekuwa wahawajitokezi kwa wingi kuwania nafasi hizo za uongozi kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo na kukatwa majina yao, kutopitishwa kwenye kura za maoni ndani ya chama, kutokana na imani iliyojengeka ni viumbe dhaifu hawawezi uongozi, na ndiyo maana wanatoa elimu kwa viongozi wa vyama vya siasa, ili kuitokomeza dhana hiyo na kumpatia nafasi mwanamke kugombea uongozi.













     Kamati ya siasa ya CCM wilayani Kishapu wakiwa katika picha ya pamoja na wanaharakati kutoka mtandao wa TGNP mara baada ya kumaliza mkutano wao, huku mwenyekiti wa ccm wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu katikati akiwa ameshika kitabu cha ilani ya uchaguzi kwa wanawake.
    Imeripotiwa na Mwandishi;Adolf Mwingira

No comments

Powered by Blogger.