Serikali Yazindua "Takukuru App" Kuthibiti Trafiki Wala Rushwa
Serikali Ya Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Imezindua App Mpya Kwa ajili Ya Kuwabaini Askari Usalama Barabarani Ambao Wanakula Rushwa.
Uzinduzi huo umefanyika Sambamba na Uzinduzi wa Kampeni Ya utatu yenye lengo la kuongeza mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa barabarani kwa kushirikisha Takukuru, Jeshi la Polisi na wadau mbalimbali.
Mfumo huo wa ‘Takukuru App’ utawezesha wananchi kutuma taarifa za vitendo vya rushwa zinazotokea sehemu mbalimbali nchini kwenda Takukuru.
Mwananchi atakuwa na uwezo wa kupakuwa na kuwa nao mfumo huo kwenye simu yake ya mkononi, utamuwezesha kuonesha eneo ambapo tukio la rushwa linafanyika, kutoa ufafanuzi wa tukio lenyewe ili maofisa wa Takukuru waweze kufuatilia, kisha atatuma ujumbe huo kwenda Takukuru na kupewa mrejesho wa kupokewa kwa ujembe alioutuma.
Faida nyingine ya mfumo huo utaliwezesha Jeshi la Polisi kuona taarifa hizo na kufanya uchunguzi kisha kutoa mrejesho wa hatua zilizochukuliwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, amewataka wananchi kutoa taarifa za ukweli kupitia App hiyo bila kuwaonea watu ambao wana visa nao kwa mambo binafsi.

Hata hivyo Mkuu wa jeshi la polisi (IGP) Simon Sirro Amesema matumizi ya teknolojia Ya habari na mawasiliano(TEHAMA) yatasaidia kupunguza Vitendo Vya rushwa barabarani.
No comments
Post a Comment