Shirika la Boeing lakumbwa na hatari ya kukabiliwa na suala la usalama wa ndege zake
Shirika la Boeing linakumbwa na hatari ya kukabiliwa tena na suala la usalama wa ndege zake baada ya vifusi kupatikana kwenye tengi za mafuta katika ndege kadhaa ambazo zilikuwa zinasubiri kuwasilishwa kwa wanunuzi.
Msimaizi wa ndege aina ya Boeing 737, amewaambia wafanyakazi wake kwamba ugunduzi huo ni jambo lisilokubalika.
Msemaji wa shirika la Boeing amesema kwamba kampuni hiyo haikugundua tatizo hilo na kusababisha ndege hizo kuchelewa zaidi kuanza tena huduma zake.
Hilo linawadia wakati ambapo ndege aina ya 737 Max bado hazijaidhinishwa kurejea kutoa huduma baada ya kusababisha ajali mbili mbaya ambapo abiria walipoteza maisha.
Shirika hilo la Marekani lilisema kwamba limegundua vifusi vilivyoachwa ndani kwenye matenki ya fueli kwa ndege kadhaa za 737 Max ambazo hazijawasilishwa kwa wateja.
Msemaji wa kampuni hiyo aliiambia BBC: "Wakati tunazikagua na kuchunguza ndege za 737 Max vile zilivyo kabla ya kuziwasilisha, tukagundua vifusi. Hilo likachangia kufanyika kwa ukaguzi upya tena wa kina na kufanyia mfumo wake marekebisho mara moja."
Vifusi hivyo ni kama vile uchafu, vifaa vya metali na vingine vilivyoacha na wafanyakazi wakati inaunganishwa.
Ugunduzi huo ni wa haivi karibuni zaidi katika msururu wa matatizo yanayokumba shirika hilo la ndege ambalo wakati fulani lilikuwa lina ndege za Boeing zenye mauzo mazuri zaidi.
Kwa sasa ndege hizo zimesitishwa kutoa huduma na wadhibiti kote duniani tangu Mwarch 2019.
Ndege hizo zilipigwa marufuku kusafiri baada ta ndege mbili kuanguka na kusababisha vifo vya watu 346.
No comments
Post a Comment