Header Ads

Header ADS

Tetesi za soka Ulaya Jumatano

 Real Madrid haitajaribu kumsajili Kylian Mbappe mwezi Januari badala yake itatupa ndoano kwa mshambuliaji huyo mfaransa mwenye umri wa miaka 22 katika dirisha lijalo la kiangazi -mkataba wake na Paris St-Germain utakapotamatika. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kiungo mchezeshaji Mbrazil Philippe Coutinho, 29, atawakacha Newcastle United mwezi Januari kwakua hana mpango wa kuondoka Barcelona. (Sport - in Spanish)

Wolves wako tayari kumuuza winga wa Hispania Adama Traore mwezi Januari wakati huu mazungumzo kuhusu mkataba mpya yakiendelea kusuasua, na klabu yake ya zamani Barcelona itachuana na Liverpool kuwania saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25. (90min)

Kocha wa zamani wa Chelsea Frank Lampard anataka kurejea ligi kuu England msimu huu akiifuatilia Leicester City iwapo Brendan Rodgers ataondoka kwenda kurithi mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer pale Manchester United. (Eurosport)

Wayne Rooney anatarajia kusalia kama kocha wa Derby County lich ya " the Rams" kukatwa alama 9 zaidi na kusalia shimoni kushuka daraja baada ya kukubali kuvunja sheria za fedha. (Sun)

Real Madrid huenda ikatupa ndoano zake kwa kiungo wa Manchester United Muholanzi Donny van de Beek katika dirisha la mwezi Januari wakati huo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 atapatikana kwa ada nafuu kutokana na kukosa nafasi ya kucheza. (Fichajes - in Spanish)

Barcelona inajiandaa kuipa Red Bull Salzburg kitita cha £33.8m kwa ajili ya kumsajili Karim Adeyemi - lakini Borussia Dortmund wako kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumsajili mshambuliaji huyo Mjerumani mwenye miaka 19. (Sport1 - in German)

Burnley wako tayari nyota wake James Tarkowski amalizie mkataba wake msimu ujao kuliko kumuuza mwezi Januari - huku West Ham na Newcastle wakimtaka mlinzi huyo wa kati wa England, 28. (Football Insider)



No comments

Powered by Blogger.