Header Ads

Header ADS

Ajali yatokea Tanga

 Watu ambao idadi yao haijafahamika wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali ya mara iliyotokea katika eneo la Sindeni wilayani Handeni mkoani Tanga.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni (DC), Siriel Mchembe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema kuwa idadi kamili ya vifo na majeruhi bado haijafahamika.
Amesema kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamki leo Jumatano Machi 16, 2022.
Mchembe amesema kuwa ajali hiyo imehusisha basi ndogo la abiria aina ya Coaster na Toyota Hiace.
"Taarifa za awali zinaeleza kuwa Hiace ndio ilipasuka tairi na kupotea njia baada ya hapo wananchi walijitokeza kuangalia ajali, ikatokea Coaster ikiwagonga wananchi ambao walikuwa kwenye ajali” amesema na kuongeza:
‘Watu ni wengi hospitali wanapatiwa matibabu, kuhusu vifo idadi kamili tutasema tukimaliza uokoaji", amesema Mchembe.


No comments

Powered by Blogger.