Wanajeshi wa Kenya wauawa
Zaidi ya wanajeshi 10 wa Kenya wameuawa katika shambulio la kilipuzi kilchotegwa kando y abarabara kusini mwa Somalia
Wengine watano walijeruhiwa vibaya baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi cha kujitengenezea katika eneo la Gedo, karibu na mpaka wa Kenya-Somalia border.
Majina ya wanajeshi waliouawa hajatolewa lakini mgombea wa zamani wa urais wa Kenya ameandika katika mtandao wa Twitter kwamba ndugu yake mdogo ni miongoni mwa waliofariki.
Shambulio hilo limehusishwa na kundi la al-Qaeda lenye uhusiano na al-Shabab ambalo limefany amashambulizi kama hayo dhidi ya raia na msafara wa vikosi vya usalama.
Wanajeshi waliouawa ni sehemu ya kikosi cha walinda usalama wa Muungano wa Afrika kilichopelekwa Somalia kusaidia serikali ya nchi hiyo kukabiliana na wanamgambo wa al-Shabab.
Miezi ya hivi karibuni imeshuhudia ongezeko la mashambulio yanayolenga maeneo ya umma, mitambo ya serikali na vituo vya ukaguzi vya usalama.
No comments
Post a Comment