Header Ads

Header ADS

MCHECHU aidai "The citizen" mabilion kwa kumchafua

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu amefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania akilitaka gazeti la The Citizen kumlipa fidia ya Sh. bilioni 3 kwa madai ya kuandika habari zilizomchafua.



Katika kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa Mei 13, 2022 mbele ya Jaji Leila Mgonya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Mchechu amedai toleo la Gazeti hilo la Machi 23, 2018, lilichapisha habari iliyosomeka ‘Why JPM dissolved NHC Board, sacked Mchechu’ ikiwa na tafsiri isiyo rasmi kuwa kwanini JPM alivunja Bodi ya NHC, kumfukuza Mchechu’.

”Habari hii ililenga kunichafua, kunishushia hadhi, kunikosanisha na jamii kubwa ya Watanzania na kuonekana kuwa mimi ni mtu nisiyefaa kabisa kuwa kiongozi au sehemu ya jamii njema ya Watanzania mtu nisiye na maadili, nisiyeaminika na kimsingi nisiyestahili hata kuongoza popote,” amesema Mchechu ambaye anawakilishwa na mawakili wa kujitegemea Aliko Mwamanenge na Vitalis Peter katika kesi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.