Header Ads

Header ADS

TBS yawataka watoa huduma kuhakiki vipimo

 Kuelekea siku ya Vipimo Dunia, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewashauri watoa huduma za kijamii pamoja na wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wamehakiki vifaa vyao katika shirika hilo ili kujihakikishia kama vifaa hivyo vinakidhi ubora wa viwango vya kimataifa.


Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Metrolojia kutoka TBS, Stella Mroso wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika jijini Mwanza huku akiwakaribisha wafanyabiashara pamoja na wananchi wote kuhudhuria maadhimisho hayo ili kujipatia elimu sahihi ya vipimo.

Aidha amesema wafanyabiashara wengi hukosa fursa za kufanya kazi na mashirika pamoja na taasisi kubwa za kimataifa kwa sababu ya kukosa uthibitisho wa ubora wa viwango wa vifaa wanavyotumia hali ambayo pia inalikosesha taifa mapato.

No comments

Powered by Blogger.