Watoto wadogo kumi na tisa na watu wazima wawili wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi katika shule ya msingi kusini mwa Texas baada ya mtu mwenye silaha kufyatua risasi katika Shule ya Msingi ya Robb katika jiji la Uvalde kabla ya kuuawa na vyombo vya sheria, maafisa walisema.
Mbali na kuuawa kwa watoto wadogo kumi na tisa, watu wazima wawili wameuawa akiwemo mwalimu
Mireles, mwalimu ambaye aliripotiwa kuuawa, alikuwa na umri wa miaka 40 na alikuwa na binti chuoni, kulingana na ukurasa wake kwenye tovuti ya shule.
Alikuwa mwalimu kwa miaka 17. Ukurasa huo ulimnukuu akisema: "Ninapenda kukimbia, kupanda milima, na sasa unaweza kuniona nikiendesha baiskeli!!"
Shangazi yake, Lydia Martinez Delgado, aliambia New York Times mpwa wake "alipendwa sana" na "alikuwa mtu wa kufurahisha katika sherehe".
Maafisa wa Marekani, Maseneti na Wamarekani wengine mashuhuri wameonesha kuguswa na shambulio hilo katika shule ya msingi kusini mwa Texas. na hapa tunawaangazia kauli za baadhi yao.
Rais wa Marekani Joe Biden "Nilitarajia nitakapokuwa rais nisingelazimika kufanya hivi tena," Biden alisema, akilaani vifo vya "watoto wasio na hatia" wa darasa la pili, la tatu na la nne katika "mauaji mengine Marekani."
Wazazi wao "hawatawaona tena watoto wao, kamwe hawatakuwa anao wakiruka kitandani na kubembelezwa nao," alisema.
"Kama taifa, inatubidi kuuliza, 'Ni wakati gani katika jina la Mungu tutaacha kupigia watu risasi?'
"Lazima tuchukue hatua," alisema na kupendekeza kurejeshwa kwa marufuku ya kutumia silaha na "sheria zingine za zakawaida."
No comments
Post a Comment