Zelensky asema Urusi inaelekeza nguvu zake zote Donbas
Rais wa Ukrane, Volodymyr Zelensky, amesema Urusi inatumia nguvu zake zote kupambana kwenye miji minne ya mkoa wa Donbas, ambako kwa sasa hali mbaya sana.
Akizungumza kwenye hotuba yake ya kila usiku kwa taifa, Zelensky amesema kila chembe ya nguvu iliyobakia nayo Urusi imeelekezwa sasa kwenye miji ya Liman, Popasna, Sieviero-donestk na Slaviansk, ambako lengo ni kuharibu kila kilichopo. Hata hivyo, rais huyo wa Ukraine alisema kuwa wanajeshi wa nchi yake wanapambana kufa na kupona lakini itawachukuwa muda kuweza kushinda.
Aliwaambia raia wa Ukraine kwamba wajivunie uwezo wao wa kupambana kwa miezi mitatu mizima katika vita ambavyo wengi nchini Urusi na kwenye mataifa ya Magharibi walidhani vingelichukuwa siku tatu tu kumalizika. Zelensky alitumia hotuba hiyo kuomba silaha zaidi kutoka mataifa ya Magharibi, yakiwemo makombora na vifaru.
No comments
Post a Comment