Rais Biden amelihutubia taifa akiliomba bunge kuidhinisha sheria kudhibiti vifo vya bunduki
Rais
wa Marekani Joe Biden ametoa hotuba huko White House alhamis usiku kwa kulitaka
bunge kuidhinisha sheria za kawaida ili kujaribu kuzuia matukio ya hivi
karibuni ya vifo vinavyotokana na ufyatuaji risasi wa umma ambavyo vimewashtua
wamarekani wengi.
White House
imesema Biden alitoa wito wa masharti mapya ili kukabiliana na janga la ghasia
za bunduki ambazo zinasababisha vifo kila siku.
Haikuwa wazi kama
Biden atatetea masharti yoyote maalum ambavyo angependelea yapitishwe, kama
vile ukaguzi unaoangalia historia ya nyuma kwa wanunuzi wa bunduki, au kupiga
marufuku uuzaji wa silaha zenye nguvu ya haraka, ambazo zilikuwa zimetumika
katika ufyatuaji risasi wa umma wa hivi karibuni.
Hakuna kipengele
chochote kitakachoweza kupitishwa katika bunge lililogawanyika kisiasa ambapo
wabunge kwa miaka mingi wamekuwa wakitofautiana kuhusu sheria ya kumiliki
bunduki.
Lakini baadhi ya
wabunge wanajaribu kuweka masharti zaidi baada ya kesi tatu za ufyatuaji risasi
wa umma ndani ya kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
Watu weusi 10
kwenye duka la vyakula waliuawa kwa kupigwa risasi katika shambulizi la ubaguzi
wa rangi kwenye mji wa Buffalo katika jimbo la New York, wanafunzi 19 na
waalimu wawili waliuawa kwa risasi wakiwa darasani mwao katika shule ya msingi
ya Robb kwenye mji wa Uvalde katika jimbo la Texas, na watu wanne wengine
waliuawa katika kituo cha matibabu cha Tulsa katika jimbo la Oklahoma.
Related Posts
-
Next
Bi.Kevela: Wanawake UWT acheni kupanga safu ya uongozi
-
Previous
Kesi yanguruma Mwaikali akipinga kusimikwa askofu mpya wa Konde
No comments
Post a Comment