CHADEMA: Katibu mpya Kanda ya Kati ataja vipaumbele vitatu
Katibu
mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kati, Emmanuel
Masonga ametaja vipaumbele vitatu atakavyoanza navyo katika nafasi yake hiyo
mpya.
Hivi karibu Kamati Kuu ya Chadema ilifanya
uteuzi wa Makatibu wapya wa Kanda ambapo Masonga aliyekuwa Kanda ya Nyasa
aliteuliwa kwenda Kanda ya Kati huku aliyekuwa Kanda ya Kati,
Gwamaka Mbugi akipelekwa Kanda ya Nyasa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya ofisi
na Katibu aliyepita, Masonga amewaomba wanachama wa CHADEMA wa ya
kanda hiyo wawe na umoja na wapendane.
“Naomba tupendane mapokezi haya ni uthibitisho
kwamba hapa kuna upendo,mimi ni muumini wa ushirikiano ili tufanye mambo
makubwa kwa ajili ya chama chetu,nataka maendeleo,nataka chadema izidi kusonga
mbele”
Kwa upande wake, Mbugi amewaomba wanachama wa
chama hicho kumpa ushirikiano Gwamaka kama walivyokuwa wakimpa yeye.
“Kuna yale ambayo tulipishana naomba radhi
naondoka Kanda ya kati nikiwashukuru kwa jinsi ambavyo mmenipa ushirikiano
mkubwa nasema asanteni sana,”amesema.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Singida, Jingu
Emmanuel amewaomba Makatibu hao kutenda haki katika utendaji wao wa kazi
bila ya kumwonea mtu huku akiahidi kumpa ushirikiano Katibu mpya wa Kanda
hiyo Masonga.
Mwenyekiti wa Chadema mkoani Morogoro,
Jackson Malisa amesema anaamini mabadiliko hayo yataleta chachu ya maendeleo
kwani Makatibu hao bado ni vijana na wana kesho nyingi.
No comments
Post a Comment