CHADEMA yawapinga Mdee na wenzake
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeweka pingamizi katika maombi ya Halima
Mdee na wenzake ya amri ya muda ya Mahakama kuizuia Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) na Spika wa Bunge kuwavua ubunge.
Chama hicho kimeweka
pingamizi hilo Mahakama Kuu ambayo imetoa amri ya kuwa hadhi ya Wabunge hao
itabaki kama ilivyo mpaka siku iliyopangwa ya usikilizwaji wa pingamizi hilo,
Juni 29, 2022.
Halima Mdee na
wenzake wamefungua maombi katika Mahakama Kuu dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa
Chadema kuomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wa chama
hicho.
Pamoja na
maombi hayo ya ridhaa namba 27 ya mwaka 2022, pia wamefungua maombi ya amri ya
zuio dhidi ya NEC na Spika, kutochukua hatua dhidi ya uamuzi wa CHADEMA wa
kuwavua uanachama ambayo yaliyopangwa kusikilizwa na Jaji Mustapha Ismail.
Hata hivyo tayari
yametajwa na kupelekea mawakili wa CHADEMA kutoa pingamizi dhidi ya maombi hayo
ya zuio, ambapo inapinga usikilizwaji wa maombi hayo ikidai kiapo cha kuyaunga
mkono kina kasoro za kisheria.
No comments
Post a Comment