China yagundua kifaa cha kubaini watu wanaoangalia picha za ngono
Watafiti nchini China wamegundua kifaa maalum
ambacho kitakuwa na uwezo wa kusoma akili, mawimbi ya ubongo au mvurugo wa
kimihemko akilini wanaoupata watu hasa wanaume pindi wanapotazama picha (pilau)
au videos (connections) za ngono (X).
Kwa mujibu wa mitandao mikubwa ya China, kifaa hicho kinavaliwa kichwani na kimeanza kuonesha matokeo mazuri baada ya wanafunzi wa kiume 15 wa chuo kufanyiwa utafiti wa kuvalishwa kifaa husika mbele ya kompyuta zinazoonesha picha za kikubwa.
Taarifa hizo zinasema kuwa, kama mtu
hajatazama picha za ngono matokeo ya kifaa hicho yatakuwa tofauti na yule
ambaye ametoka kutazama, kwa hiyo kifaa husika kitasaidia kuwadaka wote wanaopenda
kutazama videos za connections ili kukomesha wimbi kubwa la watazamaji wa
videos hizo.
Nchini China kutazama connections za ngono ni
kinyume na sheria hivyo mamlaka zimekuwa zikihaha kufanya juu chini kuondoa
kabisa matumizi ya mapicha hayo machafu hasa kwa wanaume ambao tafiti
zinaonesha ndio watazamaji wakubwa ingawa hata wanawake watadakwa na kifaa
hicho ikiwa pia wametazama.
No comments
Post a Comment