Watu 22 wafariki wakila bata klabu
Takriban
watu 22, wanaume kwa wanawake, wamekutwa wamefariki dunia katika kilabu ya
usiku kwenye kitongoji cha jiji la London Mashariki mwa Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo, miili yao ilipatikana katika ukumbi wa Enyobeni Tavern na wengine kadhaa wanasemekana kujeruhiwa.
Msemaji wa polisi Brigedia Tembinkosi Kinana aliambia kituo cha habari cha Newzroom Africa kuwa mazingira iliyopelekea tukio hilo inachunguzwa kwa sasa.
"Hali
inayozingira tukio hilo inachunguzwa tunapozungumza. Hatutaki kufanya uvumi
wowote katika hatua hii," Brigedia Tembinkosi Kinana alisema.
Kinana
alisema wengi wa waliokutwa wamekufa ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 na
20.
Kamishna wa Polisi wa Eastern Cape, Nomthetheleli Lilian Mene akizungumza na SABC News alisema kwamba kulikuwa na madai ya mkanyagano ndani ya eneo hilo la burudani.
Lakini
Unathi Binqose, afisa wa idara ya jamii na usalama ya Eastern Cape, akizungumza
kutoka eneo la tukio, alipuzilia mbali mkanyagano kama chanzo cha kifo.
"Ni
vigumu kuamini kuwa ni mkanyagano kwani hakuna majeraha ya wazi yanayoonekana
kwa waliofariki," Binqose aliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya
simu.
Gazeti
moja la eneo hilo, DispatchLive, liliripoti kwamba “miili imetapakaa kwenye
meza, viti na sakafuni; bila dalili za wazi za kuumia”.
Msemaji wa idara ya afya ya jimbo la Eastern Cape, Siyanda Manana, alisema miili hiyo itasafirishwa hadi katika vyumba vya kuhifadhia maiti vya serikali ambako jamaa wanatarajiwa kusaidia kuwatambua waathiriwa.
Alisema
alielewa waathiriwa walikuwa wanafunzi waliokuwa wakisherehekea kumaliza kufanya
mitihani wa shule ya upili.
No comments
Post a Comment