DC atumia trekta kuwafikia wananchi
Mkuu
wa Wilaya ya Kilombero, Hanji Godigodi amelazimika kutumia usafiri wa trekta
kwenda umbali wa Kilometa 60 kutoka Ifakara mjini, ili kuwafikia wananchi wa
Kijiji cha Chiwachiwa kilichopo Kata ya Mbingu, wilayani Mlimba kutokana na
ubovu wa Barabara.
Wilaya
hiyo iliyopo Mkoani Morogoro inakabiliwa na ubovu wa miundombinu kwa baadhi ya
maeneo ambapo Godigodi amesema alilazimika kufika eneo hilo kutokana na
utaratibu aliojiwekea wa kutatua kero za wananchi hasa wale wanaoishi
pembezoni.
“Nikiwa
msaidizi wa Rais Samia Suluhu Hassan nina wajibu wa kutatua na kusikiliza kero
za wananchi hivyo nimeweza kusafiri kwa kilometa 60 kutoka Ifakara mjini ili
kifika kwa wananchi wa Kijiji cha Chiwachiwa lengo ni kutatua kero za
Wananchi,” amesema Godigodi.
Pamoja
na hatua hiyo pia Mkuu huyo wa Wilaya amesema, kupitia bajeti ya Serikali ya
mwaka wa fedha 2022/2023 tayari wametenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa
Barabara hiyo.
No comments
Post a Comment