Eto'o akiri kukwepa kodi akiwa Barcelona
Nyota wa kabumbu
wa Cameroon Samuel Eto'o amekiri kufanya ulaghai wa mamilioni ya dola kwenye
ulipaji wa kodi yake wakati alipokuwa akiichezea Klabu kubwa ya Uhispania
Barcelona.
Mahakama katika jiji hilo imempa
kifungo cha miezi 22 jela na faini lakini ataepuka kwenda jela kwa sababu alikiri
hatia.
Kwa ujumla, Eto'o atalazimika
kulipa zaidi ya $8m (£6.5).
Uamuzi wa mahakama ulisema Eto'o
na wakala wake walikwepa kwa makusudi ushuru wa mapato ulitokana na hatimiliki
ya picha kati ya 2006 na 2009.
Wakati wa enzi zake za uchezaji,
Eto'o alionekana kuwa mmoja wa washambuliaji bora duniani. Sasa ni rais wa Shirikisho
la Soka la Cameroon.
No comments
Post a Comment