Fiston Mayele afunga hotuba ya Bajeti Bungeni Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amewatupia Dongo mashabiki wa Klabu ya Simba nchini huku akimsifia Mshambuliaji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele kuwa mchezaji huyo anafanya nchini vizuri na amekuwa maarufu kuliko hata baadhi ya viongozi.
Mwigulu ambaye ni shabiki kindakindaki wa Young Africans amesema
hayo jana Jumanne (Juni 14) wakati akimalizia kuwasilisha hoja ya mapendekezo
ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 Bungeni jijini Dodoma.
“Nakupongeza Mheshimiwa Anthony Mavunde wewe ndio ulikuwa
Mwenyekiti wa kuisaidia Young Africans ikiwa na mapito. Nampongeza GSM kwa
kurejesha furaha ya wananchi hasahasa kwa udajili wa Fiston Mayele.
“Mayele amekuwa maarufu
kuliko Makatibu wenezi wa baadhi ya vyama vya Siasa. Nawapongeza sana na
marafiki zangu klabu ya Simba kwa kuwakilisha vyema kwenye mashindano ya
Kimataifa, wananijua mara zote kimataifa tuko pamoja, siwezi kukana Bendera ya
Taifa langu kwa ajili ya utani wa jadi,” alisema Mwigulu.
Ikumbukwe kuwa, Mayele ndiye mchezaji mwenye mabao mengi kwa
sasa kwa wachezaji wa Young Africans lakini anashika nafasi ya pili kwa
wafungaji wa Ligi Kuu mpaka sasa akiwa na jumla ya mabao 14 huku nafasi ya
kwanza ikishikwa na George Mpole wa Geita Golf FC mwenye mabao 15.
Wawili hao ndio wanatajwa kuwania kiatu cha ufungaji Bora wa
Msimu wa 2021/2022 ambayo bado mizunguko mine ili kutamatika kwa ligi hiyo
ambapo Yanga wanahitaji pointi tatu tu kutangaza ubingwa huku wakiwa na mechi
nne mkononi mpaka sasa.
No comments
Post a Comment