Simba SC: Hatuna mpango na Luis Miquissone
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC Mulamu Nghambi amesema
klabu hiyo haina mpango wa kumsajili kwa mkopo Kiungo Mshambuliaji kutoka
nchini Msumbiji na klabu ya Al Ahly ya Misri Luis Miquissone kama inavyoelezwa.
Simba SC inatajwa na kupewa nafasi kubwa kumsajili Miquissone
mwishoni mwa msimu huu, kufuatia kiungo huyo kuwa na mazingira magumu ya kupata
nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Al Ahly tangu aliposajili mwezi Julai mwaka
2021.
Mulamu amesema Simba SC haijatuma Ofa ya kumsajili Miquissone
kwa mkopo, na taarifa za kufanya hivyo wanaziona kwenye Mitandao ya Kijamii,
lakini ukweli ni kwamba hawana mpango huo.
Amesema azimio hilo linatokana na ugumu wa kumpata mchezaji
aliye kwenye vikosi vya klabu kubwa Barani Afrika, huku akizitaja kuwa ni Al
Ahly, Zamalek, Wydad Casablanca, Kaizer Chief, Orlando Pirates na nyinginezo.
“Ngumu kwa sasa kumpata mchezaji anayecheza timu kubwa zilizopo
katika Ukanda wa Afrika, hapo nazuzungumzia Al Ahly, Zamalek, Wydad Casablanca,
Kaizer Chiefs na nyinginezo.
“Hivi sasa Luis ameanza kupata nafasi ya kucheza katika kikosi
cha kwanza, hivyo ngumu kumpata kirahisi kama watu wanavypofikiria.”
“Labda itokee lakini hadi hivi sasa bado hatujapata taarifa
rasmi za kiofisi kutoka Al Ahly juu ya Luis kutolewa kwa mkopo,” amesema
Nghambi.
Miquissone huenda akaondoka Al Ahly, kufauatia Kocha Pitso
Mosimane aliyemsajili akitokea Simba SC kuondoka klabuni hapo usiku wa kuamkia
jana Jumanne (Juni 14), hivyo Kocha ajaye anaweza akashindwa kumtumia kwenye
mipango yake.
Miquissone alisajiliwa Al Ahly, baada ya kuonesha uwezo mkubwa
akiwa Simba SC kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu uliopita
2020/21.
No comments
Post a Comment