Ili kuondoa gharama za matibabu kwa watoto Wazazi/walezi wameshauriwa kuwakatia bima ya afya watoto wao
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewashauri
Wazazi na Walezi kuwakatia Bima ya Afya watoto (Afya Toto Card) kwa ajili ya
kuwaondolea gharama za matibabu pindi wanapougua ama kupata matatizo ya kiafya.
Kauli hiyo ameitoa wakati akiongea na
wananchi waliokua wakipata matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Dodoma.
Alisema wakati wanasubiri Sheria ya Bima ya
Afya kwa wote (UHC) ambayo itasaidia wananchi wote bila kujali hali zao za
maisha kupata huduma zote za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi Taifa ambapo
kutawekwa kiwango nafuu.
“Bima ya afya kwa wote itamuwezesha mwananchi
yeyote bila kujali hali yake ya maisha na ukiwa na bima hiyo utapata huduma za
matibabu pamoja na vipimo kwenye vituo vya afya hadi ngazi ya Taifa”.
Aliongeza kuwa Wizara ya Afya ipo katika
hatua za mwisho za kupitisha sheria ya Bima ya Afya kwa wote na kiwango cha
kulipia kwa mwaka kitakua ni nafuu ili kumuwezesha mtanzania kupata huduma zote
kama anazopata mtumishi wa umma ikiwepo huduma za kulazwa na vipimo mpaka
Hospitali ya Taifa.
“Wakati tunasubiri Sheria ya Bima ya Afya kwa
wote hivyo ni muhimu wazazi na walezi kuwakatia bima ya afya watoto wao kwa
gharama ya 50,400 kwa mwaka na itamuwezesha kupata huduma mpaka ngazi ya
Taifa”.
“Kwa sasa Bima hii sio lazima lakini
nitakutana na wamiliki wa shule zote za sekondari nchini katika kikao Chao ili
tuweke takwa hili la kukata bima ya Afya kwa wanafunzi wa Sekondari.” Alisema
Waziri Ummy
Hata hivyo alisema Serikali imechukua hatua
hiyo baada ya kuona watoto wakiugua mashuleni wanarudishwa nyumbani kwa ajili v
ya matibabu, hivyo akiwa na kadi yake ya Bima ya Afya itamsaidia kupata
matibabu popote awe mwanafunzi wa kutwa au wa bweni.
“Tunaanza hatua kwa hatua kama tulivyoanza
kwenye vyuo vikuu kwa mwanafunzi kuwa na bima ya Afya ya NHIF na sasa kwa
wanafunzi wa sekondari baada ya kuongea na wamiliki wa shule hizo na hata hii
ya bima ya Afya kwa wote tumesema hatutawakamata watu kwamba ni lazima pia
tunasubiri sheria ipitishwe.” Amesema Waziri Ummy
Katika hatua nyingine Mhe. Ummy Mwalimu
amewataka wauguzi katika Hospitali zote nchini kuweka mkakati mzuri wa
kuwahudumia wagonjwa kwa muda usiozidi masaa matatu kwa mgonjwa mmoja.
“Watu wanakaa muda mrefu kusubiri kumuona
daktari, nimeshamuelekeza mganga mfawidhi waliwekee mkakati, kuanzia ameingia
hospital, kumuona daktari na kufanya vipimo kwa kadri inavyowezekana.” Amesema
Waziri Ummy
No comments
Post a Comment