Marekani hapo imeelezea kusikitishwa na tetemeko kubwa la ardhi nchini Afghanistan na kusema inaangalia namna ya kuisaidia ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo muhimu na serikali ya Taliban. 

Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa rais Joe Biden, Jake Sullivan amesema Marekani imehuzunishwa mno na tetemeko hilo lililosababisha vifo vya karibu watu 1,000. 

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken amesema taifa hilo linawasiliana na makundi ya misaada ya kiutu yanayofanya shughuli zake nchini Afghanistan na yanayosaidiwa na Marekani. 

Tetemeko hilo linatokea karibu mwaka mmoja tangu rais Biden alipohitimisha operesheni ya kijeshi nchini Afghanistan na waasi wa Taliban kurejea mara moja mamlakani.