Serikali kuandaa mkakati kukomesha biashara haramu ya ujangili
Serikali
kupitia wizara ya maliasili na utalii, inaandaa mkakati utakaosaidia nchi
kuondokana na tatizo la ujangili ifikapo mwaka 2025, kupitia utekelezaji wa
mradi jumuishi wa kupambana na tatizo hilo na biashara haramu ya Wanyamapori.
Akizungumza
wakati akifungua mkutano wa tatu wa Kamati tendaji ya mradi huo leo Juni 27,
2022 uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka Amesema, lengo
la mkutano huo ni kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi na kutoa mwongozo
kwa Kitengo cha Usimamizi kuhakikisha kinafanya kazi kikamilifu ili kufikia
lengo la Serikali la kutokomeza suala la ujangili na kupambana na biashara
haramu za wanyamapori.
“Wizara
ya Maliasili na Utalii inasimamia ushirikiano kati ya washirika na wadau katika
utekelezaji wa mradi ili kufikia dira ya sera ya Taifa ya Wanyamapori
inayolenga kulinda wanyamapori na makazi yao na maendeleo ya rasilimali za
wanyamapori,” amefafanua Prof. Sedoyeka.
Aidha,
amesema mradi unalenga kupambana na ujangili kupitia kanuni za uwindaji wa
Kitalii, kuwajengea uwezo watumishi katika kupambana na ujangili, kuwawezesha
wananchi kupambana na wanyamapori wakali na waharibifu na kushiriki katika usimamizi
wa wanyamapori.
Mkutano
huo, umehudhuriwa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango
wa Maendeleo Duniani (UNDP), Wajumbe wa Kamati ya Uendeshaji wa Mradi na
Kitengo cha Usimamizi wa Mradi.
No comments
Post a Comment