Watu 130 wauawa na wanamgambo wa kiislamu nchini Mali
Watu
wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kiislamu waliua zaidi ya raia 130 mwishoni mwa
juma katika miji jirani ya katikati mwa Mali, ikiwa ni mauaji ya hivi karibuni
katika eneo hilo la Sahel lenye mzozo.
Maafisa wa eneo hilo wameripoti
matukio ya mauaji ya kiholela yaliyofanywa na watu wenye silaha huko
Diallassagou na miji miwili jirani katika eneo la Bankass, eneo la Sahel ambalo
limekuwa lenye machafuko kwa muda mrefu.
"Walichoma pia vibanda,
nyumba na kuiba ng'ombe," amesema afisa wa eneo hilo ambaye hakutaka jina
lake litajwe kwa sababu za kiusalama.
Yeye na afisa mwingine ambao wote
wawili walikimbia kijiji chao, wamesema hesabu ya watu waliouawa ilikuwa
ikiendelea Jumatatu.
Nouhoum Togo, afisa wa mji wa Bankass, mji mkubwa katika eneo hilo, amesema idadi ya waliouawa ni kubwa kuliko ile ya watu 132 iliyotangazwa na serikali, ambayo iliwashtumu wanamgambo wa kiislamu washirika wa Al-Qaeda kwa mauaji hayo.
No comments
Post a Comment