Diwani afariki ghafla msikitini
Akizungumza kwa njia ya simu Katibu wa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Busoro Pazi, alisema Marehemu Mohamed Ngonde alifariki akiwa katika Ibada ya alfajiri leo Julai 8, 2022 akiwa ibadani msikitini.
Katibu wa Madiwani Busoro Pazi amesema taratibu za mazishi bado kila wakati atakuwa anatoa taarifa baada kukaa na familia ya marehemu.
"Kwa Sasa tunafanya taratibu za kwenda kuifadhi mwili wa marehemu katika hospitali ya Rufaa Mkoa Amana "amesema Busoro.
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya
ya Ilala Said Sidde amesema taarifa za Kifo cha MH, Diwani wake Mohamed Ngonde
alifariki na taarifa alitoa Mwenyekiti wa CCM kata Majohe ambapo amesema
Marehemu Mohamed Ngonde alifariki ghafla.
Mwenezi CCM Wilaya ya Ilala Alhaj Said
Sidde amesema kila wakati taarifa kamili zitatolewa kuhusiana na msiba huo
mzito kwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wana CCM
kwa ujumla.
Alhaj Said Sidde,pia ongeza kuwa
alimwelezea Mh Ngonde kuwa kada mahiri aliyekitumikia chama cha Mapinduzi kwa
muda mrefu na kushikilia nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti serikali ya
mtaa Kichangani ,Majohe
No comments
Post a Comment