Serikali, wadau kushirikiana kuweka matumizi sahihi ya matumizi ya maji
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya maji inapaswa kuchua hatua
stahiki za kuweka mazingira rafiki ya matumizi sahihi ya rasilimali maji ambayo
inachangia kwa kiasi kikubwa pato la Taifa kuptia sekta mbalimbali zikiwemo
kilimo,mifugo, viwanda na biashara.
Hayo yameelezwa kwenye jukwaa la uhakika wa
maji lililofanyika Jijini Dodoma lililokuwa na ajenda kuu ya ufadhili wa
rasilimali fedha kwa usalama wa maji ili kuboresha maisha ya wakulima wadogo na
ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Jukwaa hilo liliandaliwa na shirika lisilo la
kiserikali la shahidi wa maji kupitia mradi wake wa utafiti wa UHAKIKA WA
MAJI((Fair Water Future ) unaotekelezwa kwenye Wilaya mbili za Kilosa na
Kilombero mkoani Morogoro,wenye lengo la kutambua uwajibikaji wa viongozi wa
Serikali katika kutatua changamoto za upatikanaji wa maji kwa shughuli za
Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Akizungumza kwenye jukwaa hilo Mwenyekiti wa
Taifa wa Bodi ya Maji Mhandisi Mbogo Futakamba alisema kuwa bado kuna uelewa
mdogo kwa wananchi juu ya mchango wa maji kwenye uchumi wa taifa hivyo kuna
haja serikali kwa kushirikiana na wadau wa maji kutoa elimu juu ya umuhimu wa matumizi
sahihi ya maji ili kuchangia pato la nchi.
Aidha amewataka wananchi kutumia fursa
zitokanzo na mabadiliko ya tabia nchi hasa katika kipindi cha mvua nyingi kwa
kuhifadhi maji ili yaweze kuwasaidia kwenye shughuli mbalimbali kama
Kilimo na Ufugaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mashahidi wa
Maji Mhandisi Herbert Kashililah amesema kuwa lengo la jukwaa hilo ni
kubadilishana uzoefu na kutoa uelewa kwa wadau wa maji kuhusu usimamizi wa
rasilimali hiyo na kuweka mkakati wa namna gani wanaweza kufanya uwekeaji
katika sekta ya maji kwa kutumia mifumo na fursa zilizopo.
Mhandisi Kashililah amesema kupitia tafiti
walizozifanya kwenye Wilaya za Kilosa na Kilombero mkoani Morogoro wamebaini
kuna mfumo unaozibana taasisi, mabonde ya maji na mamlaka zilizopewa dhamana ya
kusimamia rasilimali maji kushindwa kutekeleza na kusimamia sera na sheria
zilizopo kutokana na mgawanyo wa majukumu.
Kutokana na changamoto hiyo Mhandisi
Kashililah ameiomba serikali kufanya maboresho kwenye mfumo uliopo sasa ili
kutoa fursa kwa Taasisi na mamlaka kufanya kazi kwa uhuru hali itakayosaidia
kuweka usalama wa maji na utuzaji wa mazingira.
Tafiti zao pia zilionesha uchafuzi na
uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya maji ambao utapelekea upungufu wa
upatikanaji wa maji endelevu kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji na
uvuvi.
Naye Mkurugenzi wa uratibu wa program na
usimamizi wa mazingira kutoka Wizara ya maji Mhandisi Dorisia Mulashani amesema
kuwa jukwaa hilo limetoa fursa kwa wizara ya maji kushirikiana na wadau katika
kupata rasilimali fedha zitakazosaidia kutunza vyanzo vya maji na kuwa na
uhakika wa maji kwa taifa.
Akizungumzia mradi wa uhakika wa maji
Mkurugenzi wa shahidi wa maji Bw.Abel Dagange amesema kuwa mradi huo unalenga
kutoa elimu kwa wananchi ya namna wanavyoweza kujisimamia na kuwasilisha
changamoto zao kwa viongozi wa serikali kwa njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya
habari na kuandika barua kwa viongozi hao.
‘Kupitia mradi huo baadhi ya wakulima, wavuvi na wafugaji wa wilaya za Kilombero na Kilosa waliofikiwa moja kwa moja wamenufaika kwa kupata elimu iliyowasaidia kutatua changamoto zao zilizokuwa zinawakabili.”amesema Bw.Dagang.
Wadau mbalimbali wa maji wakifuatilia kwa ukaribu jukwaa hilo.
Mwenyekiti wa mashahidi wa Maji Mhandisi Herbert Kashililah akizungumza kwenye jukwaaa la uhakika wa maji Jijini Dodoma Taifa
Mkurugenzi wa shahidi wa maji Bw.Abel Dagange akizungumza kwenye jukwaa la uhakika wa maji lililofanyika Jijini Dodoma
Wadau walioshiriki jukwaa la uhakika wa maji wakiwa katika picha ya pamoja
No comments
Post a Comment