Wabunge watakiwa kutoa elimu ya TB kwenye majimbo yao
Mtandao
wa Wabunge Vinara wa Mapambano dhidi ya Kifua Kikuu wametakiwa kuendelea kutoa
elimu kuhusu ugonjwa huo wanaporudi majimboni.
Hayo
yamesemwa na Naibu Mwenyekiti Sebastian Kapufi wakati wa semina kwa wabunge hao
iliyoandaliwa na Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma
(NTLP)
Kafupi
alisema kuwa suala la uelewa kuhusu Kifua Kifua bado ni mdogo katika jamii
hivyo kupelekea kushamiri kwa unyanyapaa kwa wagoniwa wa Kifua Kikuu.
“Majukumu
ya wajumbe wa mtandao huo yamebainishwa ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi kwani
bado kuna uelewa mdogo kwa jamii na hivyo kupelekea unyanyapaa,” alisema
Kafupi.
Aliongeza
kuwa bado kuna uhitaji wa mikakati ya makusudi ya kudhibiti Kifua Kikuu hasa
katika maeneo ya migodi ambako wachimbaji wadogo wadogo wanapatikana.
Alisema
kwa kutoa elimu ya kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa wachimbaji hao ambao
wengi wao ni waathirika wa ugonjwa huo itasaidia jamii nzima inayowazunguka
kuelewa Kifua Kikuu kinatibika.
kwa
upande wa Meneja Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma, Dkt. Riziki Kisonga
alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuendelea kupunguza vifo
vitokanavyo na ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa asilimia 75 ifikapo mwaka 2025 kutoka
ile ya awali ya asilimia 52 ya mwaka 2020.
Aidha,
Dkt. Kisonga aliwashukuru na kuwapongeza Wabunge hao kwa kujitoa kwao katika
mapambano dhidi ya TB na kuwaomba waendelee kushirikiana na Wizara katika
kuondoa unyanyapaa uliopo kwenye jamii dhidi ya wagonjwa wa Kifua Kikuu.
No comments
Post a Comment